Monday, August 12, 2013

Fahamu aina mbalimbali na matumizi ya Wallet na handbags kwa kina dada

,
Wallet mpya kwa kina dada
 Fashion imekuwa ikikuwa siku hadi siku hapo zamani wanawake walikuwa wanabeba wallet pekee yake lakini kwa sasa wanawake wanabeba Handbags huku ndani wakiwa wameweka wallet,,
naomba leo tukumbushane mambo manne ambayo yanaweza kuwa ya msingi kwako ili kuweka mpangilio mzuri wa pochi yako 

POCHI NDOGO (WALLET)
ni vyema uwe na kipochi kidogo kwa ajili ya kuweka rangi ya mdomo(lipsticks),wanja,poda nafuta,chana na vitu vingine vilivyo muhimu kwako kuziia mpangilio mbaya wa pochi  yako.

pochi inapawswa kuwa na pesa,kadi ya benki, vitambulisho na vitu vingine ambavyo unaweza kuweka katika pochi wako hii utakufanya kufahamu vyema sehemu gani umeweka kuliko kufungua mkoba mzima na kuanza kutafuta

SIMU YA MKONONI
 fahamu ni vigumu kutembea bila simu ya mkononi kuna wanaokuwa na mbili au zaidi hivyo basi chagua sehemu nzuri ndani ya mkoba wako ili kupunguza usimbufu kuitafuta pindi inapoita au unapoiitaji. 

UFUNGUO 
hapa utakuwa wa gari au nyumba usisahau ufunguo maana utakapo upoteza utatafuta siku nzima bila nafanikio hivyo uifathi vyema katika mkoba wako sehemu nzuri .

KALAMU NA NOTEBOOK
Ndani ya pochi kunapashwa kuwepo na kalamu na notebook ilikukusaidiia kujua vitu vya kununua na pia kuorodhesha vitu ulivyo nunua kwa wale wenye tabia ya kuorodhesha vitu walivyo nunua au kupanga vitu anavyokwenda kufanya siku nzima wakati napokuwa kazini au nyumbani kalamu na notebook ni msingi sana kwako.
















No comments:

Post a Comment